Kavumbagu: Uchawi ulinirudisha nyuma
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Didier Kavumbagu, juzi alidhihirisha wazi kuwa kilichomfanya kuyumba katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara ni kuamini uchawi na mambo mengine mengi yasiyo na maana.Kavumbagu aliyecheza mzunguko wa kwanza kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kufunga mabao nane, hakuwa kwenye kiwango chake mzunguko wa pili lakini juzi aliisumbua vilivyo ngome ya Simba na kufanikiwa kufunga bao lake la 10 kwenye ligi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa aliliambia Championi Jumatatu kuwa awali aliweka fikra nyingi za uchawi kichwani mwake na mawazo mengi yasiyo na maana juu ya hatima yake klabuni hapo kutokana na kutofunga mabao ya wazi kwenye mechi kadhaa za ligi hiyo.
“Unajua mwanzo nilikuwa nikifikiria sana kuwa narogwa, ndiyo maana nikawa na msongo mkubwa wa mawazo kichwani na vile nilivyokuwa nikikosa mabao basi nikawa nazidi kuwa na ‘mastress’ mengi.
“Lakini nashukuru Mungu sasa hivi nimeanza kurudi kwenye kiwango changu cha awali baada ya kujikita zaidi kwenye mazoezi na kuachana kabisa na mastress na fikira za uchawi,” alisema Kavumbagu.
chanzo:globalpublishers.info
Posted by Unknown
on 4:43 AM. Filed under
Mcharuko wa leo,
Michezo,
Slider
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response