|

FAMILIA YA RAIS MWINYI MATATANI



FAMILIA ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi imejikuta matatani kufuatia nyumba namba 13, kitalu 33F iliyopo Mtaa wa Mwinjuma, Kinondoni, jijini Dar anayoishi mjukuu wake, Abood Hassan Mwinyi kupigwa kufuli kwa amri ya mahakama.
Tukio hilo lilijiri saa 6:11 Jumamosi ya Mei 17, mwaka huu ambapo ilidaiwa Abood anaishi kwenye nyumba hiyo na mama mkwe wake bila uhalali.
Edward Francis Bongwe ni mtoto wa aliyekuwa mmiliki na ndiye aliyeipiga kufuli nyumba hiyo akiwa ameongozana na Mjumbe wa Nyumba 10, Shina Namba 16, Zubeda Mrisho na Hariri Mohamed  anayedaiwa kuimiliki nyumba hiyo kwa sasa ambaye aliinunua kwa marehemu mzee Francis Mawenge.
Habari zinadai awali, mbali na Abood, mtoto wa Mzee Ruksa aitwaye Abbas naye alikuwa akiishi katika nyumba hiyo lakini baada ya kuuzwa kwa Hariri na kutakiwa kuhama, alitii agizo mapema kwa kwenda kuishi sehemu nyingine.
Novemba 7, mwaka 2011, Abood na Abbas walipewa notisi ya siku 90 kuhama katika nyumba hiyo chini ya Kampuni ya Uwakili ya LRK Chambers kupitia wakili wake, Richard Mmbando.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba LRK/GDM/NTC/0.045/011 iliwataka wawili hao ifikapo Februari 6, 2012 wawe wamehama lakini mpaka sasa Abood anaendelea kuishi humo huku akitambua kuwepo kwa barua hiyo.
Siku ya tukio, Edward ambaye pia ni msimamizi wa mirathi ya marehemu mzee Francis, akiwa ameongozana na Hariri na mjumbe, walimkuta mama mkwe wa Abood, Eshe Yassin ambaye alikuwa amembeba mtoto mchanga.
Alipojulishwa lengo la ujio huo, mwanamke huyo aliwazuia kutofunga kufuli mlangoni kwa vile hawakuwa na pa kwenda.
Alipoona hasikilizwi, Eshe alimpigia simu Abood na kumweleza kinachoendelea ambapo ilipofika saa 5:53, Abood alifika kwa kasi akiwa na gari dogo lenye namba za usajili T 572 BZU.
Hata hivyo, alishindwa kuingia ndani na gari hilo kwa sababu geti lilishapigwa kufuli. Akashuka na kuingia ndani ambapo alikuja juu baada ya kukuta zoezi la kupiga kufuli milango ya ndani likikaribia kuanza.
Hali ilikuwa tete na kukatokea vurugu kidogo baada ya Edward kumwamuru Abood kuhama muda huo ambapo kijana huyo alikataa kufanya hivyo, kitendo kilichoifanya familia ya marehemu mzee Francis kumfikisha mjukuu huyo wa rais mstaafu Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar.
Alifunguliwa kesi ya jinai yenye Kumbukumbu OB/RB/8741/2013 KUJIPATIA HUDUMA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi alionekana kituoni hapo muda mfupi baada ya Abood kufikishwa ikisemekana alitaka kujua kilichokuwa kikiendelea.
Kwa upande wake, Abood alipohojiwa na gazeti hili kutaka kujua kwa nini aliendelea kuishi katika nyumba hiyo wakati barua ya wakili ilimtaka awe ameondoka tangu Februari 6, 2012, alisema ana kila kitu, yaani vielelezo vya kumfanya aendelee kuishi. Hata hivyo, hakuvionesha
chanzo:globalpublishers

Posted by Unknown on 6:12 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "FAMILIA YA RAIS MWINYI MATATANI"

Leave a reply