|

KAKA, DADA WANASWA WAKIDUU




UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi ‘wakiduu’ kando ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi!

Imefahamika kwamba vijana  hao, kaka na dada (majina tunayo)  wamenaswa ‘wakiduu’ katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
TUKIO ZIMA
Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.
Risasi Mchanganyiko lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.
Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.
DEMU ALIKUWA AKIZINGUA
Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.
Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.
Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.
Ni kama vile hawakuwa na makubaliano na kile walichokuwa wakienda kukifanya.
Mara kadhaa dada huyo alionekana kumkwepa kaka yake na alikuwa akijiondoa karibu yake pale alipomlazimisha kutaka kumfanyia kitu kisichokuwa cha kawaida
KAMERA ZAELEKEZA KWAO
Kamera za Risasi Mchanganyiko ziliwafuatilia wawili hao kwa kuwa walionekana kuwa na kitu ‘spesho’.

WAINGIA MAPANGONI
Mpaka wanazama katika mapango yaliyopo kando ya ufukwe huo wa Coco, kamera zilikuwa zikiendelea kuwachukua hadi walipozama ndani kabisa ya mapango hayo.

WANASWA LIVE
Walipozama ndani ya mapango hayo, ghafla walitokea askari ambao nao walikuwa wakifuatilia nyendo za wawili hao.
Askari hao wa Kituo cha Oysterbay, wakiongozwa na kamanda wa oparesheni maalumu katika Wilaya ya Kinondoni, Kamanda Swai walifuatilia kwa umakini tukio hilo.

WANASWA
Wakiwa chini ya mapango, kaka na dada waliondoa ‘viwalo’ vilivyokuwa maungoni mwao na kuanza kuduu kama vile walikuwa katika ufukwe unaoruhusiwa kufanya vitendo hivyo.

WAKUTWA WATUPU
Kabla askari hawajawavamia, waliwashuhudia wawili hao wakiwa katika kilele cha sterehe yao huku dada mtu akionesha kutoa ushirikiano kwa shingo upande.
Ghafla, askari waliwavamia na kuwatibulia starehe yao kisha kuwatia mbaroni.

KAKA ATAKA KUFANYA FUJO
Baada ya kuona kuwa wamevamiwa na askari, kaka mtu alichomoka na kutafuta silaha ili kuweza kujihami na wavamizi wake bila ya kujua kama ni askari.
Katika hilo nusura zipigwe kati ya askari na kaka huyo ambaye alikuwa akitaka kupigana na watu asiowajua kwa kuwa walikuwa wametinga mavazi ya kiraia.
Hata hivyo, alitulizwa na kutakiwa kuvaa pensi yake ili aweze kutoa maelezo kwa kina.

DADA APIGWA NA BUTWAA
Wakati yote yakiendelea, dada mtu alikuwa amepigwa na butwaa na kutojua cha kufanya hadi aliporushiwa kitenge chake kilichokuwa pembeni ili ajisitiri mwili wake.

SIRI YAFICHUKA
Katika mahojiano ya awali yaliyoongozwa na Kamanda Swai, ilibainika kwamba wawili hao ni ndugu wa damu yaani kaka na dada.

DADA ALITOKA MKOA
Maelezo hayo yanasema kuwa dada mtu alitoka mkoani na alikuja kutembea jijini Dar es Salaam, ndipo kaka yake alipomtaka watoke kwenda kumuonesha vivutio vya jiji hilo.
“Nina miaka 19, nimetokea Iringa kuja Dar kutembelea familia lakini kaka akanileta huku na kunifanyia vile, siyo kama tulikuwa tumekubaliana,” alisema dada huyo kwa aibu.
Kaka mtu alikiri kile kilichosemwa na dada yake na kushindwa kujitetea kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani.

WASEKWA RUMANDE
Wawili hao walichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Oysterbay kwa ajili ya kufunguliwa kesi ya uzembe na uzururaji na kusekwa rumande kabla ya kufikishwa mahakamani.
chanzo:globalpublishers

Posted by Unknown on 5:42 AM. Filed under , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "KAKA, DADA WANASWA WAKIDUU"

Leave a reply