|

LULU AIBUA JIPYA

NYOTA wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, ameibua jipya ambapo kwa sasa habari ya mjini ni kwamba ana bwana mpya aliyetajwa kwa jina moja la Junior, Amani limezinasa habari hizo.
Ishu hiyo ambayo ndiyo gumzo midomoni mwa watoto wa mjini ilianza kusambaa tangu Aprili 1, 2013 staa huyo alipoangusha pati ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Serena katikati ya Jiji la  Dar es Salaam.
Maneno ya mjini yanasema kuwa staa huyo amekuwa akiweka picha yake akiwa na Junior kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wadau wakimpongeza kwa kumtambulisha mpenzi wake huyo.
Mbali na picha ya Lulu akiwa na huyo Junior, ipo picha aliyopiga mama yake Lulu akiwa na kijana huyo katika pozi la kufanana na mwanaye.
Gazeti hili halikuyaamini maneno ya wadau wala ya mjini, juzi lilimsaka nyota huyo na kumuuliza kuhusu madai hayo ya watu ambapo alikataa katakata kuwa na bwana mpya.
Msikie mwenyewe: “Junior si mpenzi wangu, ni rafiki tu na ana mchumba’ake, sema watu wamekuwa wakinihusisha naye ili niongee wakati mimi sitaki kabisa kuongelea kitu chochote hasa visivyo na maana kama hicho.”
chanzo:globalpublishers

Posted by Unknown on 6:19 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "LULU AIBUA JIPYA"

Leave a reply