MDOSI ANAYEDAIWA KUMNYONGA MWALIMU DAR... NAYE AJIUA
MHINDI mwenye uraia wa India, Srinivasa Rao Talluri, 36 anayedaiwa kumuua Mwalimu Elizabeth Mmbaga wa Shule ya Msingi Atlas, jijini Dar es Salaam amejiua Aprili 17 mwaka huu katika Hoteli ya Transit iliyopo Karakata.
Talluri ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya vinywaji vikali ijulikanayo kwa jina la Moan’s Drinks Ltd iliyopo Oysterbay, Dar maiti yake ilikutwa chumbani saa mbili asubuhi na inadaiwa alijiua kwa kunywa sumu ambayo mabaki yake yamepelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi.
Habari za kipolisi zimesema kuwa baada ya wafanyakazi wa Hoteli ya Transit jijini Dar kugundua kuwa Mhindi huyo amekufa, walitoa taarifa polisi ambao walifika na walipochunguza chumbani, walikuta kuna pombe aina ya Pushkin chupa tatu, chupa yenye sumu ya kuulia wadudu, chips na maziwa glasi moja.
Inadaiwa kwamba Mhindi huyo aliachishwa kazi katika kampuni hiyo Aprili 2, mwaka huu baada ya kugundulika kuwa alitumia vibaya zaidi ya shilingi 400,000 ambapo Aprili 3, mwaka huu alifikishwa polisi Kituo cha Oysterbay, jijini Dar.
Mwandishi wetu alifika katika ofisi za Moan’s Drinks Ltd alikokuwa akifanyia kazi Mhindi huyo na kuonana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Raju na akakiri kutokea kwa kifo cha Talluri.
Habari zinasema mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu iliyopita na ukasafirishwa kupelekwa India Jumatano ya wiki iliyopita kwa ajili ya mazishi.
Mhindi huyo anadaiwa kuwa alikuwa mpenzi wa Mwalimu Elizabeth ambaye siku moja kabla ya kifo chake imeelezwa kuwa alikuwa naye kwenye baa moja karibu na nyumba ya Eliza, hata hivyo, alikutwa amekufa katika chumba chake Kimara Baruti, Dar Aprili 15 mwaka huu huku shingoni kukiwa na michubuko iliyoashiria kuwa alinyongwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika hoteli hiyo.
“Ni kweli alikutwa amekufa katika Hoteli ya Transit na chumbani tulikuta sumu ambayo tumepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi,” alisema.
chanzo:globalpublishers
Posted by Unknown
on 8:01 AM. Filed under
Mcharuko wa leo,
Media bar,
Micharuko Mipya,
Michezo,
Siasa,
Slider
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response