|

UWOYA AJISAFISHA KUPITIA KWA RAIS


STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata. 
Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.
“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu ningeitwa na rais wa Burundi kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo maana aliniita mwaka 2011 kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu tusingekubalika hadi na viongozi wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,” alisema Uwoya akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kuhusu madai ya wasanii kuwa na tabia chafu.

Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais  Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri. 
chanzo:glalpublishers

Posted by Unknown on 3:01 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "UWOYA AJISAFISHA KUPITIA KWA RAIS"

Leave a reply