|

Lauryn Hill jela miezi mitatu


MSHINDI wa tuzo za Grammy, Lauryn Hill, amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi zaidi ya dola milioni 1 za Kimarekani ndani ya miaka 10 iliyopita.
Hill, mtoto wa watumwa wa zamani, aliyeanza kuimba akiwa mdogo miaka ya 1990 na kundi la Fugees, alikiri mwaka jana kushindwa kulipa kodi ya dola milioni 1.8 kutokana na pato lake la mwaka 2005 hadi 2007.
Hukumu hiyo iliyotolewa juzi, imehusisha pia ukwepaji wa malipo ya kodi ya kaunti za benki miaka ya 2008 na 2009 inayofanya jumuisho la dola milioni 2.3. Licha ya kulipa dola 900,000 hivi karibuni, Hill bado anadaiwa riba ya malimbikizo yake, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani imesema.

Posted by Unknown on 4:31 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Lauryn Hill jela miezi mitatu"

Leave a reply