|

USTADHI MBARONI KWA ULAWITI

USTADHI aliyetajwa kwa jina moja la Ahmad (38) anayefundisha Chuo cha Tawfiq kilichopo Kinondoni B, Dar ambaye pia ni mfanyabiashara, anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuwalawiti watoto watatu ambao ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Msisiri.

Watoto hao (majina yanahifadhiwa kwa sababu za kimaadili)  wawili kati yao ni wanafunzi wa darasa la nne na mmoja ni wa darasa la tano katika shule hiyo.
WAZAZI SOMENI KWA MAKINI HAPA
Wakisimulia kisa hicho, watoto hao walisema, Ustadh Ahmad ambaye ni Mpemba anayemiliki duka lililopo jirani na shule wanayosoma watoto hao, amekuwa na tabia ya kuwarubuni kwa juisi na keki.
Katika maelezo yao kwa mwandishi wa habari hizi, mmoja wa watoto hao alisema: “Kama mimi nilikuwa nikipita kwenda shule ananiita ndani ya duka kisha anafunga na kunipa juisi na keki.
“Mara ya pili, akanipa tena juisi halafu akanipaka sijui ni mafuta gani yale halafu akanifunga kamba mikononi na miguuni.”
Anaeleza kuwa baada ya hapo, alimfunga kitambaa mdomoni ili asiweze kupiga kelele kisha akamwingilia bila huruma na kwamba alimtishia kuwa akisema atamuua, maelezo ambayo yaliungwa mkono na watoto wote.
MWALIMU MKUU ANASEMAJE?
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msisiri, Suzan Orege alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema: “Hawa watoto walianza tabia ya utoro, ndiyo tukaamua kuwaambia waje na wazazi wao. Cha kushangaza, wazazi wakasema watoto wao huondoka kila siku nyumbani kwenda shuleni.
“Tukawapa adhabu kali na kuwauliza wanapokwenda ndipo walipomtaja huyo mwanaume. Sisi kama shule tukaamua kuripoti suala hilo polisi na tunashukuru walifika na kumchukua. Sasa tunaacha sheria ifanye kazi yake.”
Kesi ya Ahmad ipo Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar na imepewa jalada namba OB/RB/8252/2013, OB/RB/8253 na OB/RB/8253, uchunguzi unaendelea na watoto hao walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
chanzo:globalpublishers.

Posted by Unknown on 2:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "USTADHI MBARONI KWA ULAWITI"

Leave a reply