|

DEMU AMFANYIA TIMBWILI HEMED


STAA mwenye swaga za kupitiliza Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amepatwa na masaibu ya kutaka kushushiwa kipondo hevi na demu ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya kumpulizia pafyumu bila ridhaa yake.
Tukio hilo liloloonekana kumkosesha amani PHD, liliibuka Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, jijini Dar wakati staa huyo alipokuwa akizindua singo yake mpya inayofahamika kwa jina la Rest of My Life.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kilimtonya paparazi wetu kuwa wakati staa huyo akipafomu jukwaani alishika pafyumu kama swaga za kunogesha shoo huku akiwapulizia baadhi ya mashabiki wake, haswa warembo.
Aliwapulizia pafyumu baadhi ya warembo akiwa jukwaani lakini kumbe kitendo kile hakikumpendeza mdada mmoja hivi aliyeonekana kama ni shombeshombe.
“Sasa akaona isiwe tabu, akasubiri aliposhuka jukwaani, akamfuata nyuma ya jukwaa (back stage) na kuanza kumshika shati huku akihoji kwa nini alimpulizia pafyumu hiyo bila ridhaa yake,” kilisema chanzo hicho.
Wakati mwanadada huyo akiwa amemtaiti PHD, baadhi ya watu waliokuwa karibu waliingilia kati na kumsihi dada huyo apunguze munkari, zoezi ambalo lilichukua takriban robo saa.
Hemed alifanikiwa kuchomoka kwenye himaya ya mlimbwende huyo na kumwacha akiendelea kumchimba biti.
Juhudi za kumpata Hemed juzi Jumanne ili aeleze kwa undani kilichompata hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.
chanzo:globalpublishers.

Posted by Unknown on 3:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "DEMU AMFANYIA TIMBWILI HEMED"

Leave a reply