|

MASHOGA WAFURIKA PATI YA MSANII


PATI ya Miss Utalii 2004 ambaye ni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Sara Mwakapala aliyomuandalia mwanaye Anthonio kumpongeza kwa kutimiza umri wa miaka mitatu, nusu itibuke baada ya jamaa waliodaiwa ni mashoga kufurika.
Katika pati hiyo iliyofanyika maeneo ya Leaders, Kinondoni, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, mbali na mashoga hao waliokuwa wakiserebuka taarab, pati hiyo pia ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao walimtuza Anthonio fedha na zawadi kibao.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Sara alifunguka kuwa alifurahishwa na tukio hilo la mwanaye kutimiza umri huo kwani malezi si mchezo, yanahitaji kujipanga.
Sarah alimzawadia mwanaye simu aina ya Ferrari yenye thamani ya Sh. laki tano huku maandalizi yote ya shughuli hiyo yakigharimu Sh. milioni 3.
Wageni waliomtuza mtoto huyo ni pamoja na Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Mimah Mohamed ‘Baby Candy’.   
chanzo: globalpublishers

Posted by Unknown on 2:01 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "MASHOGA WAFURIKA PATI YA MSANII"

Leave a reply