|

Dereva alewa tilalila:azimika barabarani

MWANAUME mmoja aliyetambulika kwa jina la Joseph Mwaleni anayedaiwa kuwa ni dereva wa kituo kimoja cha redio Bongo (jina tunalihifadhi), alikutwa amezimika ghafla na kuuchapa uzingizi barabarani akiwa kwenye gari lake.
Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Afrikasana ambapo Joseph akiwa kwenye foleni alipitiwa na usingizi mzito na magari yalipoanza kutembea gari lake liliendelea kusimama hali iliyosababisha foleni kuwa kubwa ndipo walipotokea wasamaria wema wakalisukuma mpaka pembeni huku njemba huyo akiwa amelala fofofo.
Baada ya kusogezwa pembeni, msamaria mwema alimpekua mifukoni, akachukua simu yake na kumpigia mmoja wa watu aliowasevu ambaye alifika eneo la tukio na ndiye alitoa maelezo kuwa jamaa huyo alikuwa dereva wa kituo hicho cha redio.
“Huyu jamaa amelewa kupitiliza kwanza ukimnusa hivi unasikia harufu ya pombe tu, tumemtoa katikati ya barabara na amshukuru Mungu kwa sababu amekutana na sisi wasamaria wema,” alisema shuhuda mmoja.

Posted by Unknown on 4:14 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Dereva alewa tilalila:azimika barabarani"

Leave a reply