|

ALIYEMFUMANIA MKEWE GESTI AGEUZIWA KIBAO!


LILE sakata la hivi karibuni la mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Asha kudai kumfumania mshikaji wake aitwaye Beda Mloka mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam akiwa na mkewe gesti, lililoripotiwa na gazeti ndugu na hili la Risasi Mchanganyiko, limechukua sura mpya kufuatia aliyefumania kugeuziwa kibao na aliyedaiwa kufumaniwa.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba jina lake lisiandikwe gazetini juzi kililitonya Ijumaa kuwa, mara baada ya fumanizi hilo lililotokea katika gesti iitwayo Pumzika iliyopo Msimbazi Center kisha aliyefumaniwa kuchezea kichapo, mambo yalikwenda chinichini lakini juzikati aliyefumania aliitwa Kituo cha Polisi, Pangani.
“Lile tukio lilikuwa gumzo sana pale mtaani kwetu, na kwa aibu Beda alitoweka kwa siku kadhaa lakini juzi Baba Asha akaitwa polisi, inavyoonekana mgoni kamgeuzia kibao mwenzake
“Nilijaribu kudadisi nikasikia Beda anadai Baba Asha na mkewe wamemchezea chezo na anajaribu kuonesha kuwa hakufumaniwa, kitu ambacho kinawashangaza wengi kutokana na mazingira waliyokutwa gesti,” alidai mtoa habari huyo.
Katika kujua ukweli wa sakata hili, mwandishi wetu alimtafuta Beda bila mafanikio lakini Baba Asha alipopatikana alisema: “Ni kweli leo (Jumatano ya juzi) niliitwa pale Polisi Pangani, jamaa niliyemfumania na mke wangu kaenda kunishitaki kuwa nimemfanyia mchezo.
“Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana, yaani kanitibulia ndoa yangu halafu ananigeuzia kibao! Tutaona sasa yeye na mimi nani ataumbuka. Nimetakiwa kwenda kuripoti tena pale polisi kesho (jana) na baada ya hapo nitajua nini cha kufanya.”
chanzoL:globalpublishers

Posted by Unknown on 4:11 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "ALIYEMFUMANIA MKEWE GESTI AGEUZIWA KIBAO!"

Leave a reply